Foster Excellence and Integrity

UCHANGANUZI LINGANISHI WA HAKI ZA MWANAMKE KATIKA TAMTHILIA KILIO CHA HAKI NA KIMYA KIMYA KIMYA

Authors

, AKANKUNDA ELIZABETH

Abstract:

Utafiti huu unachunguza linganishi ya haki ya mwanamke katika tamthilia ya Kilio Cha Haki na Kimya Kimya Kimya. Utafiti huu ambao ni utafiti linganishi uliongozwa na malengo mahususi matatu ambayo ni moshi,kubainisha haki za mwanamke katika tamthilia mbili teule, pili , kueleza nafasi ya mwanamke katika tamthilia teule.Tatu , kufafanua uhusiano uliopo katika tamthilia Kilio Cha Haki na Kimya Kimya Kimya kuhusu haki za mwanamke na lengo ku ni kuchunguza ulinganishi wa haki za mwanamke katika katika tamthilia teule. Katika kutekeleza malengo hayo mtafiti aliteua sampuli ya utafiti kwa mbinu ya kusudio. Sampuli hoyo ndiyo iliyotumiwa kukusanya data na data hizi zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya upitiaji wa nyaraka na kusoma kwa makini na kuchambuliwa kwa mkabala wa kimaelezo .Matokeo yay a utafiti huu yameonyesha kwamba,waandishi wa tamthilia teule tukianzia na Alamin Mazrui yeye anaonyesha mwanamke Lanina anayesababisha mgomo katika mapambano ya makaburu ya wafanyakazi wa shamba la Delamon ili wagunduwe haki zao dhidi ya udhalimu wa makaburu na unyanyasaji. Pia mwanamke anapewa gaki ya upiganiaji wa haki , uzazi, ulezi ujasiri na ujenzi wa familia.Na kwa upande wa Said A Mohamed yeye anadhihilisha kijana kike kijasiri aitwaye Mpya anao sababisha mapinduzi na kuleta mabadiliko katika nchi yake yenye uongozi wa ubinafsi dhidi ya kukimya kwa muda mrefu.isitoshe anaelza haki za mwanamke kuwa utiifu, uzalendo , ukombozi, ushujaa na uvumilivu. Pili utafiti huu umeonyesha kuwa mwanamke ana nafasi kadhaa kwa mfano mtetezi wa haki za usawa, mlezi mjenzi wa familia, msimamo thabiti, mzazi mzalendo mpenzi ,mchochezi ,mvumilivu, na msaliti kulingana na waandishi hawa wa tamthilia teule na vile vile katika uhusiano. Tatu matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa waandishi wa tamthilia teule pamoja wametumia haki za mwanamke katika kazi zao kwaani uzazi, ujenzi wa familia , utetezi haki za usawa, uongozi na uzalendo katika kufikisha ujumbe waliokusudiwa na jami zao muafaka na jamii walioandikia.

Download FULL PDF